KAULI YA RAIS MAGUFULI KUHUSU TUNDU LISSU KUPIGWA LISASI
Thursday, 7 September 2017
Comment
Rais John Magufuli, amesema amepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Katika akaunti yake ya Twitter, Rais Magufuli amesema anamuombea Lissu kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka.
“Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria,” amesema.
Lissu amejeruhiwa leo Alhamisi mchana akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.





0 Response to "KAULI YA RAIS MAGUFULI KUHUSU TUNDU LISSU KUPIGWA LISASI"
Post a Comment
TOA MAONI SIO MATUSI